Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Bunda ikiongozwa na Mwenyekiti Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Dkt. Vicent Anney imekutana kwa lengo la kutoa maoni kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 katika Ukumbi wa Heriet. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitoa Utangulizi ya kuwa lengo la Kikao hicho ni kufahamu malengo ya Dira ya Taifa 2050 lakini zaidi kutoa ushauri na mapendekezo ya nini kifanyike kufanikisha malengo hayo ya Taifa.
kabla ya Kutoa maoni yao wajumbe walipitishwa kwenye Dira ya Taifa ya 2025 na kisha kusomewa na kufahamishwa malengo ya Dira ya Taifa 2050. Wajumbe waliridhishwa na malengo yaliyomo katika dira hiyo, lakini pia walitoa mapendekezo yao kulingana na asili ya Wilaya ya Bunda nini kikifanyika Dira hiyo ya 2050 itafanikiwa kwa asilimia kubwa. Maoni yote yaliyotolewa na wajumbe yalipokelewa.
Baadhi ya Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ni;-
i. Kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi Jumuishi unaopunguza umasikini, unaozalisha Ajira na kuchochea mauzo ya Biashara nje ya nchi.
ii. Kuongeza na kuimarisha matumizi ya Teknolojia hasa ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
iii. Kuongeza uzalishaji wa Viwanda na kuimarisha huduma Bora za Kijamii kwa wote
iv. kuweka msukumo wa Uongozi tija katika uzalishaji na Uongezaji Thamani sekta za Kilimo,Ufugaji, Uvuvi, Misitu na Madini
v. Kuongeza ubora wa Elmu na Mfunzo katika ngazi zote
Mbali na maoni yaliyotolewa Ukumbi, wajumbe walielekezwa pia njia ya Mtandao na Simu ya Kutoa maoni. Kupitia Tovuti Mtanzania anaweza kutoa maoni kupitia https://dira2050portal.planning.go.tz au kupitia Simu kwa kupiga *152*00 mwisho unaweka alama ya Reli kisha utachagua namba 8 - 4 na kufuata maelekezo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda