Halmashauri ya Mji wa Bunda imepokea mifuko 400 ya saruji kutoka kampuni ya Mwanza huduma, kukamilisha maboma ya sekondari ili kuongeza miundombinu na kutengenza mazingira wezeshi ya kujifunzia.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo fupi ya kupokea saruji, Bi Lydia Simioni Bupilipili Mkuu wa Wilaya ya Bunda, ameipongeza sana kampuni ya Mwanza huduma kwa msaada mkubwa iliyoutoa wa mifuko 400 ya simenti kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Bunda hasa katika idara ya elimu. Amesema watoto wetu wanahitaji mazingira rafiki ya kujifunza ikiwa ni pamoja na kukaa katika madarasa mazuri na yaliyo bora.
Hata hivyo, Mwakilishi wa Mwanza huduma alisema kampuni hiyo imechangia maendeleo katika mikoa mbalimbali na wataendelea kuchangia maendeleo kutokana na faida wanayoipata ili kurudisha shukrani kwa jamii na ameiomba Halmashauri kutumia simenti hiyo mifuko 400 kama iliyokusudiwa.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth P. Mayanja aliwashukuru kampuni ya Mwanza huduma kwa msaada wa mifuko 400 itakayosaidia kukamilisha miundombinu ya sekondari mpya nne ambazo ziko katika hatua za mwisho za ukamilishaji katika kata ya Bunda stoo, Nyatwali na Mcharo. Mkurugenzi ameahidi kuitumia simenti hiyo kama ilivyokusudiwa na amewashukuru wadau wote wanaondelea kuchangia shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo kwani hiyo ndiyo njia ya kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa vitendo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda