KATIBU Mkuu Tamisemi Eng. Joseph Nyamhanga, amesema Serikali iko mbioni kutafuta fedha zaidi ya Shilingi Milioni 700 za Kitanzania kwaajili ya ukarabati wa Kituo cha Afya cha Manyamanyama ili kipewe hadhi ya kuwa Hospitali kama ulivyompango wa Serikali kila Halmashauri kuwa na Hospitali.
Ameeleza hayo leo tarehe 22/04/2020 alipotembelea Kituo cha afya cha Manyamanyama baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Peter Mayanja kuwasilisha ombi kwake kusaidia upatikanaji wa fedha za kuboresha kituo cha afya cha Manyamanyama na kukipandisha hadhi kuwa Hospitali ya Halmashauri.
Aidha, Mkurugenzi amesema kuwa kituo kinakabiliwa na uhaba wa miundombinu kama jengo la X-ray, Jengo la OPD, jengo la Mortuary, upungufu wa wodi, jengo la dharura ( Emergency room) na Uzio kuzunguka kituo, ukizingatia kituo hiki kinahudumia watu wengi sana na wengine kutoka nje ya mipaka yake.
Katibu Mkuu amefanya ziara ya siku moja ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda, kwa kutembelea Sekondari ya Kabasa na Kituo cha afya cha Manyamanyama. Aidha amewapongeza sana viongozi wa Halmashauri na Wilaya kwa kazi kubwa wanaiyofanya ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayotolewa na serikali.
Imetolewa na:
Kitengo cha Afisa Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Mji wa Bunda
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda