Jumatano, 02.08.2023
Katika kuhakikisha kazi inafanyika ipasavyo, leo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Msalika Robert Makungu ametembelea shule za Msingi na Sekondari kuangalia majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa EP4R, BOOST, SEQUIP na GPE LENS kuangalia ubora wa majengo hayo ambayo ni madarasa pamoja na maabara.
Shule za Msingi zilizotembelewa ni Bunda A, Bunda B, shule ya msingi Miembeni A, shule ya msingi Nyerere na shule mpya ya msingi inayojengwa katika kata ya Nyasura.
Kwa upande wa shule za Sekondari RAS ametembelea shule ya Sekondari Migungani, Nyamakokoto na Bunda stoo. Lakini pia alipata nafasi ya kutembelea kituo cha Kujifunza kwa Walimu Balili (Cluster).
Katibu Tawala amepongeza ubora wa majengo hayo na kutoa maelekezo mbalimbali katika maeneo yenye mapungufu ili yaweze kufanyiwa kazi. Aidha amezitaka shule zote kuilinda na kuitunza miradi hiyo kwa maendeleo ya watoto na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel Mkongo amesema wanachukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa mara kwa mara kutembelea miradi hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Aidha, Mkongo ameahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Katibu Tawala kuhakikisha yanatekelezwa kwa wakati.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda