Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndg. Gerald Musabila Kusaya ameongoza kikao Cha Maandalizi ya kilele Cha siku ya kupinga ukatili dhidi ya Wazee Duniani ambapo Kitaifa maadhimisho haya yatafanyika katika Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara tarehe 15.06.2024.
Kikao kimejumuisha Kamati ya Usalama ya Wilaya, Watalamu kutoka Mkoani na Wilaya ya Bunda pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo wakikilishi wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mara na Kamati ya Ushauri ya Wazee Mkoa wa Mara.
Maadhimisho haya yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Miembeni na kutanguliwa na Bonanza la Michezo pamoja na Kongamano litakalokua na mada moto moto kuhusu wazee.
Jiandae kushiriki bila kukosa siku itakapofika. Taifa limetuheshimisha wakazi wa Mkoa wa Mara kuadhimisha Kitaifa nasi tuoneshe kwamba wameleta nyumbani. Karibuni sana.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda