KIKAO Cha Kwanza Cha Maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Bunda kimefanyika Leo chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Dkt. Vicent Anney Mkuu wa Wilaya ya Bunda kupanga na kupitia Maandalizi ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kuingia Wilaya ya Bunda tarehe 02.08.2024 na kuondoka tarehe 04.08.2024 kuelekea Mkoa wa Simiyu.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda: tarehe 02.08.2024
Halmashauri ya Mji wa Bunda: tarehe 03.08.2024
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amezielekeza Idara zenye miradi kuanza Maandalizi mapema na kuweka miradi katika hali inayotakiwa.
KAULI MBIU: Tunza Mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu".
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda