Timu ya Watalamu kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Watalamu kutoka Mradi wa TACTIC imefika katika Halmashauri ya Mji wa Bunda leo kufanya Tathimini na Mapitio ya Miradi pendekezwa itakayojengwa na Mradi wa kuboresha Miji na Majiji (TACTIC).
Katika Kikao hicho kilichofanyika pamoja na wajumbe wa Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na Kamati ya Halmashauri ya Uratibu wa Mradi huu imepitia miradi inayopendekezwa ambayo ni Barabara kilomita 3, Soko na Stendi ambayo katika hatua ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu ndio miradi itakayoguswa.
Watalamu wamesema miradi iliyopendekezwa imelenga miradi inayogusa moja kwa moja mahitaji ya wananchi kwa asilimia kubwa.
Baada ya Kikao Wajumbe wote walikwenda kutembelea miradi hiyo kuangalia uhalisia wake.
Lengo Kuu la Kikao hiki ni kuwa na uhakika wa miradi itakayofanyiwa kazi ili kuepusha mabadiliko ya Miradi wakati mradi ukiendelea kutekelezwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda