“Viongozi wa dini mnamchango mkubwa sana wa kuelimisha wananchi kuchanja chanjo ya UVIKO – 19, kwasababu katika sehemu za ibada ndio sehemu pekee ambazo wengi tunakimbilia kupata faraja kutoka kwa viongozi wetu wa dini”.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel Mkongo wakati akifunga Kikao cha Viongozi wa dini Wilaya ya Bunda pamoja na Wataalamu wa Afya kutoka Mkoani na Wilayani kwa kushirikiana na Wadau wa AMREF. Kikao hiki kililenga kujadiliana namna ya kudhibiti maambukizi ya Uviko – 19 ikiwa ni pamoa na kufanikisha mpango harakishi na shirikishi kwa jamii na utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19.
Mkongo amewaomba viongozi wa dini wakati wakihubiri, kufundisha na kutoa elimu kwa waamini wao, kuhamasisha kupambana na maambukizi ya UVIKO – 19 hasa kuchanja ili kujiweka salama.
Mkurugenzi ameongeza kuwa, Tafiti kutoka kwa wataalamu wa afya zinaonesha kuwa kirusi hiki hakina nguvu kwa watu waliochanja ikilinganishwa na watu wasiochanja ambapo inakua hatari zaidi.
Kwa upande wao viongozi wa dini wamefurahishwa sana na elimu waliyopewa kutoka kwa Wataalamu wa afya na kuazimia kwenda kuelimisha na kuwahamasisha waamini wao kupima na kuchanja chanjo ya UVIKO – 19.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda