Halmashauri ya mji wa Bunda kwa kuona umuhimu wa kuwajengea uwezo watendaji wa serikali kwa ngazi zote mwaka wa fedha ilitenga fedha kwajili ya mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wake, ilikufanikisha lengo lake la kutoa huduma bora kwa wananchi wake. mafunzo hayo yaliyo funguliwa na Mkuu wa wilaya ya Bunda Bi. Lidia Bupilipili yana lengo la kukuza uelewa kwa washiriki pia kuwawezesha kusimamia fedha za umma kwa weledi. akifungua mafunzo hayo mkuu wa wilaya amewataka waheshimiwa madiwani kuwamakini katika mafunzo ili wakitoka waweze simamia vyema fedha za maendeleo katika kata zao. Awali Mkurugenzi wa Mji bi Janeth akimkaribisha mkuu wa wilaya aliwashukuru wawezeshaji toka chuo cha Serikali za Mtaa(Hombolo) kwa kuitikia wito na kukubali kuja kuwzesha jamii na watendaji katika Halmashauri ya mji. Aidha alieleza kuwa mafunzo hayo yatashirikisha wakuu wa idara na vitengo, waheshimiwa madiwani, watendaji wa kata, mitaa na vijiji wa halmashauri.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda