Halmashauri ya Mji umepokea pikipiki 10 kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo kupitia Ofisi ya Rais Tamisemi.Pikipiki hizo wamekabidhiwa waratibu wa elimu kata 10 awali waratibu 3 Tu ndio walikua na pikpik hivyo sasa kata 13 ambazo zinashule zinapikpiki hivyo utendaji utaimarika.Halmashauri inamshukuru Mh Rais hakika Bunda Tc haitamuangusha tunashukuru saana. Akikabidhi pikipiki hizo august 3, 2018 mkurugenzi wa Mji Bi. Janeth P. Mayanja amewaasa maofisa hao kutumia pikipki hizo kwa malengo yaliyo kusudiwa ili kuongeza ufanisi na ustawi wa elimu.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda