Halmashauri ya Mji wa Bunda chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Michael Kweka imefanya Mkutano wa Baraza la Madiwani sehemu ya kwanza kwa kuwasilisha taarifa za Kata robo ya tatu tarehe 13.05.2024 ambapo Waheshimiwa Madiwani wamewasilisha mafanikio na changamoto zilizopatikana katika Kata zao kwa kipindi Cha robo ya Tatu.
Baadhi ya Mafanikio waliyoyataja ni pamoja na Serikali kuendelea kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwezo Madarasa, Maabara pamoja Zahanati. Kuhamasisha Jamii kushiriki katika shughuli za Maendeleo ikiwa ni pamoja na kuibua miradi mipya katani.
Aidha, Waheshimiwa Madiwani wameiomba Serikali kuendelea kukamilisha miradi inayoibuliwa na Wananchi na kufikia sifa au vigezo vya kukamilishwa na Serikali na pia wameiomba Serikali kutoa kwa wingi Ajira hasa za Walimu wa Sayansi kwani shule nyingi bado zinauhitaji licha ya Jamii kuendelea kuajiri walimu wa muda.
Kwa upande mwingine Waheshimiwa Madiwani wameiomba Ofisi ya Mkurugenzi kuijulisha Mamlaka ya mawasiliano kuboresha mawasiliano katika baadhi ya Maeneo ambayo mtandao unashika kwa shida na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Bunda kuboresha huduma ya Maji kuwa ya uhakika na kufikishwa katika Maeneo ambayo maji hayajafika
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Juma Haji Juma ameeleza kupokea na kuyafanyia kazi yale yanayogusa Ofisi yake na kuweka msisitizo kwa Watendaji kutekeleza majukumu yao.
Sehemu ya pili ya Baraza ambayo ni Mkutano wa wazi kwa wananchi wote utafanyika siku ya Jumatano tarehe 15.05.2024.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda