Aliyekua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo Leo amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mkurugenzi mpya Bwn. Juma Haji Juma. Hii ni kufuatia mabadiliko ya kiutawala yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwabadilisha Vituo Wakurugenzi hao.
Mkongo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati pale ambapo atahitajika lakini pia amemjulisha Mkurugenzi mpya kuwa Uongozi na wafanyakazi wote wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri hivyo hatopata shida katika utekelezaji wa majukumu yake.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na kusainiwa pia na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Michael Kweka ambae amemshukuru aliekua Mkurugenzi Emmanuel Mkongo kwa mchango wake alioutoa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wakati akihudumu kama Mkurugenzi na kumtakia Kila lakheri katika majukumu yake mapya.
Aidha Mheshimiwa Mwenyekiti amemkaribisha Ndg. Juma Haji Juma ambaye ndie Mkurugenzi mpya wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kuahidi yeye pamoja na Baraza lake kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wanawatumikia vizuri wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Juma Haji Juma ameshukuru kwa Mapokezi mazuri na kuahidi kushirikiana vizuri na Baraza la Halmashauri, Menejimenti na wafanyakazi wote wa Halmashauri ya Mji wa Bunda katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao sawa ikiwa ni pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Tukio hili pia limeshuhudiwa na Mheshimiwa Emmanuel Malibwa Diwani wa Nyamakokoto na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Elimu na Afya pamoja na baadhi ya Wakuu wa Idara kama wanavyoonekana katika picha.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda