Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Mheshimiwa Chacha Robert Maboto leo ametembelea na kukagua shule mpya ya Sekondari ya kata ya Bunda Mjini. Mheshimiwa Maboto ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuleta fedha kwaajili ya ujenzi wa Sekondari hiyo kutokana na maombi aliyoyafikisha Kata ya Bunda Mjini pekee ndio ilikua imebaki Haina shule ya Sekondari.
Akizungumza na wananchi, Mheshimiwa Maboto amesema licha ya Kata ya Bunda Mjini kukosa eneo la kujenga shule, ameishukuru Kata ya Bunda stoo kwa kukubali kutoa eneo katika Kata yao na kuwapatia Kata ya Bunda Mjini kujenga Sekondari hiyo.
Aidha kupitia Mkutano huo, Mheshimiwa Maboto ameahidi kutoa mashine mbili kubwa za kudurufu mitihani (Photocopy mashine) ambazo atazikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ili shule zote zipate fursa ya kuweza kudurufu mitihani yao bure na kufanikisha malengo ya kutoa Elimu Bora kwa wanafunzi kwa kupata mazoezi ya kutosha katika mitihani yao.
Mbali na hayo, Mheshimiwa Maboto amesema Bado Serikali inaendelea kuleta fedha za kutosha kwaajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa sekta ya Elimu na Afya.
Naye Diwani wa Kata ya Bunda Mjini Mheshimiwa Mzamil Kiwanila, ameishukuru Serikali pomoja na jitihada za Mbunge Mheshimiwa Robert Chacha Maboto kwa kuwezesha Kata ya Bunda Mjini kupewa fedha kiashi Cha shilingi milioni 584 kwaajili ya ujenzi wa Sekondari na kusema itanufaisha watoto wote wa Bunda.
Awali Viongozi wa Chama na Serikali, akiwemo Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda, Mwenyekiti wa UVCCM na Katibu wake wa Wilaya ya Bunda, Waheshimiwa Madiwani pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wametoa neno la shukrani kwa Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya ya kufikisha Bungeni shida na kero za wananchi, kuzipambania na kuhakikisha zinafanyiwa kazi.
Mwisho, Viongozi wote wamemshukuru Mbunge kwa jinsi anavyowagusa wananchi wake kwa kuwawezesha kiuchumi kama vile madereva Bajaji na bodaboda pamoja na makundi mbalimbali ya wajasiliamali wadogo ndani ya Jimbo la Bunda Mjini.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda