Mgogoro wa ardhi uliozuka katika eneo linalotarajiwa kujengwa makao makuu ya TANAPA kanda ya Magharibi maeneo ya Balili watatuliwa kwa Amani. Mgogoro huo ulikua baina ya TANAPA dhidi ya Bwana Malugo na Bwana Ngei waliokuwa wakigombea eneo lilillopakana na kiwanja cha TANAPA.
Awali Bwana Ngei alisema kuwa alinunua eneo hilo tangu mwaka 1997 kutoka kwa Bwana Emmanuel na kudai kua mpaka wa eneo lake ni mti na mawe yasiyohamishka yaliyopo katika katika eneo. Mzee Malugu alitoa ufafanuzi wa eneo hilo kuwa halikuwa la Bwana Emmanuel kama Bwana Ngei anavyodai bali lilikua la mzee Maduhu na alilinunua kwa maandishi.
Aidha, baada ya mvutano wa muda mrefu, Wazee wote wawili waliamua kukubaliana na kuufuta mgogoro huo na kusema kuwa eneo hilo ni mali ya TANAPA na Mzee Malugu ameahidi kulilinda dhidi ya wavamizi watakaotaka kulivamia.
Mwisho, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja ametoa pongezi kwa wazee hao kwa kumaliza mgogoro huo na kuomba Amani itawale katika eneo hilo
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda