Leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya Boost katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Lengo la ukaguzi huu ni kuangalia ubora wa madarasa yaliyokamilika na kuangalia maendeleo ya ujenzi kwa shule ambazo bado ujenzi unaendelea.
Shule ambazo zimekaguliwa ni Shule ya Msingi Ihale, Shule ya Msingi Mazoezi, Shule ya Msingi Mugaja, Shule ya Msingi Kamkenga, Shule ya Msingi Bigutu na Shule mbili mpya za Msingi moja ya kata ya Bunda Stoo na nyingingine ya Kata ya Nyasura.
Aidha Mkurugenzi ametoa maelekezo kwa maeneo ambayo hayaridhishi ili yarekebishwe kwa kuzingatia ubora na thamani za miradi hiyo.
Mbali na shule, Mkongo alitembelea pia ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kuangalia maendeleo ya ujenzi wake.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda