Akijibu hoja ya maombi timu ya Bunda Queens kupata eneo la uwanja wa michezo wa Manyamanyama kujenga kiwanja cha michezo, Mkurugenzi Emmanuel Mkongo ameeleza kuwa Mwenyekiti wacTimu aliandikiwa barua ya kujibu maombi ya Timu ambapo alijibiwa kwamba anatakiwa kufuata utaratibu kwa kuwasilisha Andiko la kina kwa Halmashauri na kwamba iwapo Halmashauri itaridhia kumpatia eneo hilo basi atatakiwa kupangishwa na kulipa kodi au ataingia ubia na Halmashauri katika uwekezaji wa uwanja huo.
Mkongo ameongeza kuwa hata kama Timu itakuwa na nia ya kupata eneo tofauti na uwanja wa Manyamanyama, Halmashauri ipo tayari kutoa ushirikiano ambapo mchakato wa fidia lazima uzingatiwe kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za ardhi.
Mkurugenzi Mkongo ametoa angalizo kwamba kuanzia sasa maombi yoyote ufadhili, uwekezaji na utoaji wa misaada unaolenga taasisi za Serikali utashughulikiwa baada ya kuwasilisha maombi rasmi kutoka katika ngazi za Kata na Mitaa na ushauri kutolewa katika ngazi ya Halmashauri.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda