Leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ndg. Juma Haji Juma amekutana na Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa lengo la kujitambulisha na kuweka mikakati ya kusafiri pamoja katika kuwatumikia wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Hii ni baada ya mabadiliko ya Kiuongozi yaliyofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwabadilisha Vituo vya kazi baadhi ya Wakurugenzi akiwemo Ndg. Juma Haji Juma aliehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kuja kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda akipokea kijiti Cha Mkurugenzi Emmanuel Mkongo alihamishiwa Manispaa ya Morogoro.
Akiongea katika kikao hicho Ndg. Juma Haji Juma amesema anapenda kuona kila mtumishi anawajibika katika nafasi yake bila kusukumwa wala kufuatiliwa. Lakini pia ameielekeza timu ya mapato na Idara zinazokusanya mapato kuhakikisha wanakusanya kikamilifu mapato na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Aidha ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa watumishi ili kuhakikisha dhamira ya Utoaji huduma Bora kwa wananchi inafikiwa. Katika hilo ameomba kuboresha mahusiano na mawasiliano ya mara kwa mara pale inapohitajika bila kusahau haki na stahiki sawa kwa watumishi wote katika Idara.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda