Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo leo amepanda miti katika viwanja vya Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa lengo la kuonesha mfano kwa Watumishi kuendeleza tabia ya upandaji miti.
Mkongo amesema ni wakati mzuri sasa wa kupanda miti katika Ofisi zetu, nyumbani kwetu na maeneo mengine yote yanayotuzunguka kwasababu ni kipindi ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
Hivyo Mkongo ametoa wito kwa Watumishi wote pamoja na wakazi wa Bunda Mji kuendeleza Utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yetu
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda