Leo umefanyika Mkutano wa Baraza la Halmashauri Robo ya nne kuwasilisha Taarifa za Utekelezaji ngazi ya Kata ambapo Waheshimiwa Madiwani waliwasilisha taarifa na kujadiliwa.
Kila Mheshimiwa Diwani alipata wasaa wa kuwasilisha taarifa za Miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika na inayoendelea kutekelezwa katika kata zao, Changamoto na kutoa maoni ya nini kifanyike kuhakikisha Halmashauri inafanya vizuri katika kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Emmanuel Mkongo alitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizotolewa na Waheshimiwa madiwani lakini pia alitoa taarifa ya fedha ambazo tayari zimeshatumwa kwa baadhi ya kata za miradi mbalimbali kama nyumba za watumishi, madarasa na miradi mingine ambayo itaanza kutekelezwa kuanzia sasa.
Hii ni siku ya kwanza ya Mkutano huu, kesho kikao kitaendelea kwa siku ya pili ambapo kitakua ni kikao cha wazi na wananchi wote wanakaribishwa kuja kusikiliza.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda