Leo Halmashauri ya Mji wa Bunda chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa bunda Mhe. Michael Kweka imefanya Mkutano wa Baraza la Halmashauri kuwasilisha taarifa za utekelezaji robo ya kwanza Julai - Septemba 2023 ngazi ya kata.
Waheshimiwa Madiwani kwa mujibu wa sheria na kanuni za vikao waliwasilisha Taarifa za utekelezaji katika maeneo yao. Baada ya mawasilisho waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kutoa mapendekezo na ushauri juu ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo inayopelekwa na Serikali katika kata zao.
Waheshimiwa Madiwani pia wameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta miradi mikubwa maendeleo katika kata zao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo amelieleza Baraza kuwa Serikali inajitahidi kuleta miradi ya mendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu na pia amesema Serikali inapambana kuhakikisha inamalizia miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa na Wananchi.
Jambo la Msingi ambalo Mkurugenzi amelisisitiza kwa waheshimiwa Madiwani ni kuhakikisha maboma ya madarasa, zahanati na nyumba za watumishi zinazoanzishwa kujengwa na wananchi zinafikia hatua ya kupokelewa na Serikali kwaajili ya umaliziaji.
Kesho siku ya pili ya Mkutano tarehe 09.11.2023 utafanyika Mkutano wa wazi wa Baraza kueleza shughuli zilizofanywa na Halmashauri kwa kipindi chote cha robo ya Kwanza. Wananchi wote mnakaribishwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda