Leo Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda limefanya Mkutano wa wazi robo ya kwanza kueleza shughuli zilizofanywa katika kipindi Cha robo ya kwanza 2022/2023 chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Michael Kweka.
Taarifa ya utekelezaji robo ya kwanza kutoka TARURA na BUWSSA ziliwasilishwa katika Baraza Hilo.
Kupitia maswali ya papo kwa papo kuhusu ujenzi wa stendi, Baraza limeeleza kuwa kupitia Mradi wa TACTIC taarifa zinaonesha kuwa mradi huo utaanza mwishoni mwa Mwaka huu kwa kutambulisha mradi na kuwajengea uwezo Wananchi.
Baraza limeeleza pia kuhusu mchakato wa kutwaa eneo la Nyatwali kwa manufaa ya Umma na Hifadhi kwamba kupitia Baraza la Mawaziri Serikali imetoa maamuzi ya kutwaa eneo hilo na tayari hatua mbalimbali za kutoa Elimu kwa Wananchi zimeanza kuandaliwa.
Baraza pia kupitia Meneja wa TARURA Eng. Baraka limeeleza kuwa zoezi la kutengeneza Barabara zilizomo kwenye mpango wa bajeti hii unaendelea na kwa Barabara ambazo hazipo kwenye mpango zitapewa kipaumbele katika bajeti ijayo.
Kuhusu udhibiti wa upoteaji wa Mapato, Baraza limeeleza kwamba saivi Kuna timu Maalumu ambayo imeundwa kusimamia na kuchunguza upotevu wa Mapato hasa ya vifusi vya madini Kata ya Kabasa.
Katika Sekta ya Elimu Baraza limeeleza kuwa saivi Serikali inatekeleza Miradi mikubwa ya kujenga madarasa yatakayopokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza 2023 na kwa upande wa maboma hasa yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi, Halmashauri ilishafanya tathimini na kutumia taarifa Wizarani kwaajili ya kutengewa fedha ya umaliziaji.
Aidha Baraza limeendelea kuwaondoa hofu Wananchi wote walioathiriwa na wanyamapori waharibifu na ambao fedha zao zilikuja mara ya kwanza na kurudi kuwa Halmashauri inafatilia jambo Hilo kwa ukaribu Wizarani na pindi litakapokamilika Wananchi hao watalipwa fidia zao.
Kwa upande mwingine, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kupitia Katibu Tawala wa Wilaya Bw. Salum Mtelela imesisitiza Umoja na Mshikamano miongoni mwa Waheshimiwa Madiwani pamoja na Watendaji. Aidha Katibu Tawala amewakumbusha Waheshimiwa Madiwani kuendelea kusimamia kwa ukaribu Miradi ya ujenzi wa Madarasa inayoendelea sasa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda