Mheshimiwa Michael Kweka Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ameongoza Mkutano wa Mwaka wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo wajumbe wa Baraza, wageni waalikwa pamoja na wananchi waliojitokeza wamepata fursa ya kujua masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo Halmashauri ya Mji wa Bunda imefanya kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.
Wajumbe wa Mkutano walipata wasaa wa kutoa maoni katika nyanja mbalimbali zinazogusa Halmashauri hasa katika usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Waheshimiwa Madiwani wamesema ni lazima Baraza na Wataalam wa Halmashauri wote kwa pamoja kushirikiana kusimamia miradi ili kuepusha sintofahsmu zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzingatia maelekezo na miongozo inayotolewa.
Aidha, wajumbe wameshauri Kamati za ujenzi kupewa elimu ya uelewa wa mambo wanayotakiwa kuzingatiwa wakati wa kusimamia miradi hususani masuala ya manunuzi. Zaidi wajumbe wameshauri kuweka vigezo vya ubora wa ujenzi vinavyotakiwa kufuatwa katika miradi yote ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bw. Emmanuel Mkongo amekili kupokea maoni na ushauri uliotolewa na wajumbe wa Mkutano na pia alitoa ufafanuzi kwa baadhi ya mambo yaliyohitaji ufafanuzi likiwemo suala la ununuzi wa vigae katika shule mpya za msingi zinazoendelea kujengwa.
Jambo lingine kubwa na la muhimu lililofanyika ni Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri na Wenyeviti wa Kamati za kudumu za Baraza la Halmashauri.
Makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Mheshimiwa Marongo Mashimo Diwani wa Kata ya Nyatwali
Matokeo ya Uchaguzi wa Wenyeviti wa Kamati yalikuwa kama ifuatavyo:
Kamati ya Huduma za Jamii-Uchumi, Elimu na Afya amechaguliwa Mhe. Emmanuel Malibwa Diwani wa Kata ya Nyamakokoto.
Kamati ya Mipangomiji na Mazingira amechaguliwa - Mheshimiwa Mzamil Kilwanila Diwani wa Kata ya Bunda Mjini
Kamati ya Maadili amechaguliwa - Mheshimiwa Mhigi Samson Shalya Diwani wa Kata ya Mcharo
Wajumbe wawili walioteuliwa Mheshimiwa Mohonda Nyahimo (Diwani wa Kata ya Kabarimu) na Mheshimiwa Edina Machibya Diwani viti maalum.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda