"Hali ya Usafi wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji wa Bunda hairidhishi" Maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda katika Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda robo ya nne 2022/2023.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda ameelekeza kutozwa faini kwa mujibu wa sheria kwa watu wote wataokutwa na uchafu mbele ya nyumba zao na wanaotupa taka hovyo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ameelekeza kufanyika oparesheni ya watu wanaotumia mifuko ya plastiki iliyokatazwa na Serikali na kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria kwani wamekua wazalishaji wakuu wa taka mjini.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Dkt. Vicent Anney ameliekeza Baraza kwa kushirikiana na watumishi kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ili kufikia asilimia zilizowekwa.
Katika hilo, Mkuu wa Wilaya amesema bila kufikia shabaha ya ukusanyaji mapato basi Baraza linakua halina uhalali wa kuwepo. Zaidi ameshauri kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato kama mifumo isiyorasmi inayotumika kukusanya mapato, magari ya mizigo yanayotorosha mizigo bila kulipa ushuru stahiki na kuhakikisha mapato yote yanaingia Halmashauri.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda