Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney amemtembelea shuleni mwanafunzi aliemkuta akijisomea barabarani usiku huku akitumia mwanga wa Taa za barabarani wakati huo huo akiuza karanga.
"Juzi nilipokua napita kwa mguu mitaani majira ya saa mbili na nusu usiku kuangalia nini kinaendelea mjini. Tangu kuwekwa kwa taa za barabarani kumefanya wananchi wengi kuwa wajasiliamali, wanauza mihogo, mahindi ya kuchoma, samaki wa kung'aa na mboga mboga kwa kutumia taa za barabarani lakini nikakuta mwanafunzi ambae nae alikua anauza karanga na huku akijisomea kwa kutumia taa za barabarani." DC. Anney
Mkuu wa Wilaya amesema jambo hilo lilimtafakarisha kiasi Cha kuamua kumtafuta kujua ni kwanini anajisomea barabarani. Mbali na kumtembelea Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amempatia Zawadi mtoto huyo zawadi ya madaftari, begi la shule pamoja na kalamu za kuandikia ili kumpa motisha ya kuendelea kusoma na kutimiza malengo yake.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemlipia mwanafunzi huyo chakula shuleni kwa mwaka mzima na ameahidi kukutana na wazazi wa Binti huyo ili kuona namna gani ya kuweza kumsaidia ili awese kufika mbali kwenye Elimu yake.
Kwa upande wake Furaha Hamis, mwanafunzi aliepewa zawadi na Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemshukuru sana Dkt. Anney kwa zawadi alizompatia ambapo amesema zitamsaidia kuendelea kufanya vizuri katika masomo yake na ameeleza ndoto zake hapo baadae ni kuwa Rais.
Mbali na zawadi alizopewa mwanafunzi Furaha Hamis, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewapa pia wanafunzi wanaosoma nae kalamu mbili mbili ili kuwapa motisha ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Furaha Hamis ni mwanafunzi wa kidato Cha Kwanza katika shule ya Sekondari Nyamakokoto. Anaishi na Wazazi wake ambao ni Wakulima. Furaha anaamini Elimu ndio itakayomsaidia kutimiza ndoto zake.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda