Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mheshimiwa David Silinde (Mb) amefanya ziara ya kutembelea Miradi ya ujenzi wa Madarasa katika Halmashauri ya Mji wa Bunda ambapo amezipongeza Halmashauri ya Mji wa Bunda kutekeleza Miradi hii kwa ubora na kuzingatia thamani ya Miradi hiyo.
Mheshimiwa Silinde ametembelea shule mpya ya Nyamakokoto inayojengwa kwa ufadhiri wa Mradi wa SEQUIP ambapo ujenzi umefikia hatua ya umaliziaji na pia ametembelea shule ya Sekondari Bunda.
Mheshimiwa Silinde amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamilia kuondoa odha ya upungufu wa madarasa Nchini na Hivyo kuwafanya wanafunzi kusoma katika Mazingira mazuri.
Zaidi Naibu Waziri ameiagiza Halmashauri ya Mji wa Bunda kuhakikisha inakamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu za Wananchi katika Sekondari ya Nyamakokoto. Aidha amewahakikishia Wananchi kwamba maboma hayo yatakamilika kwani fedha Zipo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Joshua Nassari ameishukuru sana Serikali kwa kulete fedha za kutosha kwa ujenzi wa Madarasa ya Sekondari na kujenga shule mpya mbili Moja Halmashauri ya Mji na nyingine Halmashauri ya Wilaya.
Mheshimiwa Nassari amesema ujenzi wa Shule mpya ya Nyamakokoto itaenda kusaidia Kata zaidi ya Moja hapa Mjini zenye watoto wengi. Zaidi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaleta fedha nyingi sana za miradi jambo ambalo halijawahi kufanyika hapo nyuma.
Mheshimiwa Michael Kweka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa Miradi mingi anayoileta Bunda Mji.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bw. Emmanuel Mkongo amesema Siri ya kufanya Vizuri katika Miradi inayoletwa na Serikali Bunda Mji ni Umoja, Mshikamano na ushirikiano baina ya Watumishi pamoja na wawakilishi wa Wananchi ambao ni Waheshimiwa Madiwani kupitia baraza la Halmashauri.
Mkurugenzi ameongeza kusema kuwa tayari Ofisi imetenga zaidi ya Shilingi Milioni 20 kwaajili ya kuendelea kukamilisha ujenzi wa Shule Mpya ya Kata ya Nyamakokoto.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda