Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Said Mtanda ametembelea miradi ya ujenzi wa Elimu katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na kuwapongeza wa simamizi wa miradi hiyo kwa kuhakikisha ubora wa miradi unazingatiwa.
RC Mtanda amesema nia ya Serikali kuleta miradi hii ni kuboresha miundombinu ya Shule za Msingi kupitia mradi wa Boost.
Mkuu wa Mkoa amesisitiza ushirikishwaji wa Walimu wote katika mradi, Kamati zinazoundwa zifanye kazi yao ipasavyo lakini pia jamii inayozunguka mradi huo lazima ishirikishwe itambue mradi uliopo katika eneo lao.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa shule zote za Mkoa wa Mara kuzingatia Uwajibikaji, Utawala bora na Usimamizi wa walimu katika majukumu yao na kufanya kazi kwa bidii. Zaidi amesisitiza utoaji wa adhabu uzingatie sheria na kanuni za Elimu zilizowekwa na idadi ya vikobo inayotakiwa.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Dkt. Vicent N. Anney amesema Kamati ya Usalama ya Wilaya huwa inatembelea miradi hiyo mara kwa mara kuhakikisha miradi inakamilika kwa ubora na kwa wakati. Na pia ametoa ahadi ya kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuhakikisha yanazingatiwa na kufanyiwa kazi.
Miradi iliyotembelewa ni Ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo shule ya msingi Miembeni, ujenzi wa shule mpya ya kata ya nyasura, ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo shule ya msingi Mazoezi pamoja na ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya Msingi Mazoezi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda