Licha ya hali ya hewa leo kugubikwa na mvua, haikuwazuia wananchi wa Kata ya Mcharo kufanya Mkutano wa timu ya Watalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na Watalamu kutoka Taasisi ya TARURA na BUWSSA.
Mkutano huu ulilenga kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata ya Mcharo ambapo Wananchi walipata wasaa wa kueleza kero zao ikiwa ni shida ya Maji, Barabara, fidia kwa Wanyamapori, upungufu wa walimu na Zana za kufundishia pamoja na kero nyingine mbalimbali.
Baada ya kuwasilisha kero zao, wananchi waliweza kupatiwa majibu kutoka kwa Watalamu kadili ya Kila mmoja alivyoguswa.
Mwisho Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Mcharo ambaye ndie aliekua Mwenyekiti wa Mkutano huo, aliushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kutenga muda wa kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero za wananchi wa Kata hiyo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda