Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent N. Anney ameeleza utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Bunda yenye Thamani ya shilingi Bilioni 210 katika Majimbo yote ya Wilaya ya Bunda kwa kipindi Cha Julai Disemba 2023.
Hayo yamesemwa katika Kikao Maalum Cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda imetembelea Miradi 31 sawa na Asilimia 16 ya Miradi 196 iliyotekelezwa.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema;-
"Halmashauri ya Mji ya Bunda imetekeleza miradi yenye Thamani ya shilingi Bilioni 6.01 katika sekta mbalimbali ya Kilimo na Mifugo, Elimu, Afya, TASAF na Maeneo mbalimbali ya kijamii."
"Halmashauri ya Wilaya ya Bunda imetekeleza Miradi yenye Thamani ya shilingi Bilioni 8.12 katika sekta mbalimbali."
"TRA Bunda imekua Kinara wa ukusanyaji wa Mapato ambapo imekusanya zaidi ya Bilioni 1.8 sawa na Asilimia 137. Niwapongeze walipa Kodi wa Bunda kwa kutoa Kodi kwa weledi na kwa wakati."
"RUWASA imetekeleza miradi yenye Thamani ya Bilioni 6.11 katika Maeneo mbalimbali ya jimbo la Mwibara na Jimbo la Bunda pamoja na ujenzi wa bwawa la mifugo la mihingo."
"BUWASA imetekeleza miradi minne yenye Thamani ya shilingi Bilioni 13 katika Maeneo ya Kunzugu, Ushashi - Misisi, Manyamanyama - Mugaja, Balili - Kunzugu pamoja na Rubana."
"Serikali imetumia zaidi ya Bilioni 175 kutekeleza miradi ya umeme katika Maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bunda."
"TARURA imetekeleza miradi yenye Thamani ya shilingi Bilioni 2.9 kwa Jimbo la Bunda Mjini na Jimbo la Bunda na Mwibara shilingi Bilioni 3.8."
"TAWA imeendelea kupambana na wanyama waharibifu na kuleta usalama wa watu na Mali zao katika Maeneo yanayozunguka hifadhi ya Serengeti."
"Mamlaka ya utoaji Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inaendelea kutoa vitambulisho na tumerahisisha kutoa huduma kwa kutembelea majimbo yote matatu siku moja moja ili kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi."
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda