Tarehe 07.02.2023
Baraza Maalumu la mapitio ya utekelezaji wa shughuliza TARURA kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na Mpango na Bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Halmashauri ya Mji wa Bunda limefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mwenyekiti wa Baraza hilo Mheshimiwa Michael Kweka baada ya kufungua baraza alimkaribisha Meneja wa TARURA Mhandisi Baraka Mkuya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji na Mpango na Bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhandisi Baraka Mkuya amelieleza Baraza kuwa TARURA Wilaya ya Bunda imekisia kutumia jumla ya shilingi Bilioni 4.7 kwaajili ya matengenezo ya barabara katika Halmashauri ya Mji wa Bunda ikiwa ni bajeti yenye ukomo.
Mhandisi Baraka amesema mpango na Bajeti huo ni rafiki kwasababu umezingatia maoni na vipaumbele vya Waheshimiwa Madiwani ambao kwa hakika wametoa ushirikiano wa kutosha katika kuonesha mahitaji katika maeneo yao ya Utawala. Japo ameongeza kusema kuwa mapendekezo ya Waheshimiwa Madiwani yalikua ni mengi hivyo kwa kazi ambazo zitabaki zitazingatiwa kwa mwaka wa fedha ujao.
Baada ya kuwasilisha taarifa hiyo washeshimiwa Madiwani waliongezea maoni juu ya barabara ambazo zipo katika maeneo yao ambazo wanatamani zifanyiwe kazi. Mhandisi Baraka aliyapokea maoni yao na kuwakaribisha katika Ofisi yake kwa majadiliano zaidi.
Mwisho Baraza limempongeza Mhandisi Baraka pamoja na jopo lake katika kuhakikisha wanatatua changamoto za barabara katika Mji wa Bunda. Baraza kupitia Waheshimiwa Madiwani wamekili kwamba sasaivi kazi zinazofanywa na TARURA zinaonekana katika maeneo yote.
Awali Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Bunda Paul Mohamed Mhehe ametumia fursa ya kikao cha Baraza hilo kuwasilisha ujumbe muhimu wa program ya "TAKUKURU - Rafiki" kwamba ni programu iliyoanzishwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ili kuongeza ushiriki wa kila mwananchi na wadau katika kukabiliana na Rushwa katika Utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda