Idara ya Elimu ya Awali na Msingi ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kupitia mradi wa shule bora imeendesha mafunzo ya kuimarisha ushirikiano baina ya wazazi na walimu mashuleni.
Afisa Elimu Mwalimu Said Ramadhan amesema lengo la mafunzo haya ni kuhuisha au kufufua umoja wa Walimu na wazazi shuleni hasa katika suala la ufundishaji na ujifunzaji.
Mwalimu Saidi amesema umoja huu utakapoimarika utakua ni chombo muhimu kwasababu utashiriki katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza mashuleni kama vile kukomesha utoro, kupambana na suala la ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zinazoathiri ufundishaji na ujifunzaji wa watoto mashuleni.
Aidha ameongeza kusema kuwa, umoja huu utasaidia pia kuboresha miundombinu ya ufundishaji na ujifunzaji mashuleni ikiwemo vyumba vya madarasa, vyoo pamoja na nyumba za walimu kupitia vikao mbalimbali watakavyokua wakifanya kubaini na kutatua changamoto zinazojitokeza mashuleni.
Suala lingine ni kushiriki katika Utoaji wa huduma mbalimbali kama vile chakula kwa wanafunzi mashule ili kuwafanya watoto wawe na nguvu na uwezo wa kupokea wanayofundishwa na walimu wao.
Kwa upande wa Wenyeviti kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya shule ya msingi Kitaramaka Bwn. Magerengo Mashauri amesema anaishukuru sana Serikali kwa kuleta mafunzo hayo na kuwakusanya kwa pamoja walimu na wazazi kwani hapo nyuma hayakwepo. Bwn. Magerengo anasema hapo nyuma kulikua na migogoro mingi kati ya Walimu na wazazi lakini kupitia semina hii mambo hayo yote yatakwisha na ufaulu kwa watoto utapanda.
Naye Mwalimu David Makene Mwalimu Mkuu wa shule ya Kangetyutya kata ya Wariku kwa niaba ya walimu Wakuu walioshiriki mafunzo haya anasema semina hii imekuja kuamsha ari mpya ya usimamizi utekelezaji wa majukumu ambayo kwao walimu Wakuu wanapaswa kuyafanya.
Lakini pia ameongeza kusema kuwa kuwaunganisha Walimu wakuu, Waratibu Elimu kata pamoja na Wenyeviti wa Kamati za shule utasaidia sana kujenga mahusiano mazuri katika utekelezaji wa majukumu.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda