Katika Kikao cha Lishe robo ya tatu cha kueleza utekelezaji wa Afua za Lishe, Kikao kimeazimia kutoa msisitizo kwa shule zote za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Mji wa Bunda kuendeleza Elimu ya kujitegemea kwa wanafunzi kuzalisha mazao ambayo yatasaidia kupata chakula shuleni.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Juma Haji Juma amesema mbali na kuendeleza Elimu ya kujitegemea, Idara ya Kilimo itoe ushirikiano wa kutosha katika shule hizo kwa kutoa elimu na ushauri wa Kilimo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, Idara zimeeleza jinsi shule zinavyotekeleza Afua za Lishe ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya matunda, kuanzisha bustani mashuleni, kuhimiza wazazi kuchangia chakula cha watoto wao na kuhamasisha wamiliki wa mashine wanafunga vifaa vya kuchanganyia virutubisho Lishe.
Mwisho Idara zote zinazohusika na Lishe zimeelekezwa kutenga na kutumia Bajeti ya Lishe kwa wakati.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda