Akijibu swali lililoulizwa na Diwani wa Kata ya Bunda Mjini Mhe. Mzamil Kilwanila, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bw. Emmanuel Mkongo amesema tayari wameshapokea Wataalam wanaotekeleza mradi wa kuboresha miundombinu ya Barabara, Stendi ya Kisasa, soko la kisasa, Dampo na Machinjio katika hatua ya maandalizi.
Mkurugenzi amesema lengo la ujio wa Wataalam hao lilikua kujadiliana ni miradi ipi ianze katika hatua ya awali ambapo miradi iliyochaguliwa ni Stendi Mpya, Soko la Kisasa na Kilometa kadhaa za barabara ya lami.
Mkurugenzi ameongeza kwa kusema kuwa Wataalam hao wameahidi kurudi kuanza kazi ya upembuzi yakinifu kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha 2023/2024.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda