Jumatatu 21.08.2023
Siku ya leo Wanufaika wa Mfuko wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania (TASAF) katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wamepewa elimu ya jinsia katika uzalishaji mali. Jinsia ni mahusiano ya kijamii na kiutamaduni yanayozingatia mgawanyo wa majukumu kati ya mwanaume na mwanamke.
Walengwa wameelezwa ili kufikia mafanikio ni lazima waondokane na dhana potofu ya kutenga majukumu kwamba haya wanatakiwa kufanya wanaume na yale wanatakiwa kufanya wanawake badala yake washirikiane kwa pamoja katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Aidha walengwa wamekumbushwa baadhi ya majukumu ambayo wanaweza kufanya wote kwa pamoja kama kubaini walengwa wapya, kufuatilia maendeleo ya Elimu na Afya kwa watoto, uibuaji wa miradi, kufanya maamuzi pamoja kuhusu matumizi ya Ruzuku au fedha walizopokea kutoka TASAF na kufanya pamoja shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Baada ya somo hilo walengwa wameahidi kushirikiana ili kuboresha kipato cha familia zao.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda