Ziara ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney imeendelea kuwa yenye mafanikio na matumaini makubwa sana kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Leo ilikua zamu ya kata ya Nyasura ambapo wananchi wa kata hiyo wamefunguka ya moyoni kwa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kutaka wasaidiwe.
Miongozi mwa mambo waliyoomba kusaidiwa ni kukomeshwa kutozwa fedha hospitalini kwa mama wajawazito pamoja na watoto chini ya miaka mitano, kuomba kuimarishwa kwa ulinzi na usalama, kuboreshewa huduma ya upatikanaji wa maji pamoja na kushusha bei ya maji, kuomba kituo cha Polisi kurahisisha huduma, upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa, michango mashuleni na mengine mengi.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amejibu kero za wananchi, kwa kuanza amewataka wazazi kutokomeza ukatili kwa wototo na kuwa karibu nao, kutunza vyakula walivyonavyo, kuwasomesha watoto wao na kuchangia chakula shuleni, amewataka viongozi wa makanisa kudhibiti kelele makanisani, ametoa maelekezo kwa Halmashauri hadi kufikia tarehe 20.08.2023 soko la Nyasura senta liwe limehamishwa na kuhamia soko la Manjebe.
Aidha, mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bunda kufuatilia lawama zilizotolewa za kuwatoza fedha wajazito na watoto chini ya miaka 5. Na pia amewataka wananchi kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo.
Naye Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Bunda Mjini Bi. Esther Gilyoma amesema Bunda kwasasa haina shinda ya maji kwani wanazalisha maji mengi kuzidi watumiaji na pale huduma ya maji inapokua inakosekana inakua imetokea hitilafu ndogo hutatuliwa kwa muda mfupi au umeme kukatika.
Lakini pia kuhusu bei ya maji Mkuu wa Wilaya pamoja na Meneja wamesema BUWSSA inazalisha maji mengi kuliko watumiaji na gharama za uzalishaji ni kubwa kutokana na mitambo inayotumika. Hivyo bei inaweza kupungua watumiaji wakiongezeka.
Mwisho ametoa maelekezo kwa jeshi la Polisi kuongeza doria katika maeneo yote kupunguza uhalifu.
Wananchi wamefurahi kutembelewa na Mkuu wa Wilaya na kutatuliwa kero zao zote.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda