Jumatatu, 14.08.2023
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney akiongozana na Balozi wa Pamba nchini Bwana Aggrey Mwanri, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwana Emmanuel Mkongo wametoa semina elekezi kwa Watendaji wa Kata wa Wilaya ya Bunda kuhusu utekelezaji wa majukumu yao kikamilifu.
Hayo yamejitokeza kukutokana na ziara ya Balozi wa Pamba Bwana Aggrey Mwanri aliyoifanya Wilayani Bunda kwa lengo kuwaweka tayari watendaji kupokea na kutekeleza kwa usahihi kampeni ya Mashamba darasa ya pamba yanayotarajiwa kuanzishwa katika kila kata ili kuleta matokeo chanya ya kilimo cha pamba.
Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney amewakumbusha Watendaji wa Kata kuhusu majukumu yao ya kwamba ndio Viongozi wa Kata na Viungo kwa viongozi wengine wote waliopo katani na kushughulia masuala yote yanayohusu Kata lakini pia ndiyo wahamasishaji wakuu wa masuala ya maendeleo katani ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kilimo cha pamba kinatekelezeka kwa usahihi na ufanisi.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewakumbusha Watendaji kwamba Mkubwa ni mtu yeyote anayefuata utaratibu katika nafasi yake.
Amesisitiza kuwa Mtendaji wa Kata ana wajibu wa kutatua shida, kero na matatizo yote yanayotokea katani na kwa yale yanayokuwa nje ya uwezo wake kuyawasilisha katika sehemu husika.
Kwa upande wake Balozi wa Pamba Bwana Aggrey Mwanri ameeleza kuwa suala la kusikiliza na kutekeleza maelekezo toka kwa viongozi wao ni la lazima. Ni lazima kila mmoja aheshimu mamlaka iliyojuu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa na nchi.
Balozi wa pamba aliongeza kuwa ili kufikia lengo la Wilaya kulima na kuvuna Tani elfu 28, ni lazima kila mmoja atekeleze wajibu wake katika nafasi yake.
Awali, Afisa Usalama wa Wilaya ya Bunda Bwana Fadhiri aliwakumbusha Watendaji wa Kata kuwa ni wajibu wao kusimamia utaratibu katika Kata zao na pia ni lazima watumie mbinu mbadala kuweza kuhakikisha Sheria, Taratibu na Kanuni zote zinafuatwa katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa zao la pamba katika maeneo yao.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda