Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda Ndg. Mayaya Abraham Magese amewataka Watumishi wa Serikali wa Wiyala ya Bunda kutokua na hofu katika utekelezaji wa majukumu yao hasa pale Chama kinapokua kinafuatilia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Maeneo yao.
"Chama na Serikali sote kwa pamoja tunajenga nyumba moja kwasababu Serikali inatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Sisi hatufanyi kwaajili ya kumtafuta nani mbaya bali tunaelekezana na kukumbushana pale ambapo mambo hayaendi vizuri ili kuhakikisha Ilani ya Chama inatekelezwa vizuri." Amesema Mwenyekiti Mayaya.
Hayo yote yamejili leo katika Kikao Cha Majumuisho ya ziara ya kutembelea Miradi ya Maendeleo iliyofanywa na Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Bunda kuanzia tarehe 16 - 18/05/2024.
#kaziiendeleee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda