Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. George Simbachawene Katika majumuisho ya ziara yake wilayani Bunda ambako alitembelea maeneo kadhaa yanayopendekezwa kujengwa jengo la makao makuu ya mji wa Bunda, alibaini kuwa Mji wa Bunda uko eneo sahihi na hakuna haja ya kuendelea na mchakato wa kujengwa jengo la Ofisi ya makao makuu. Aidha kaelekeza kuwa halmashauri ya Wilaya ya Bunda ipishe majengo yote kwajili ya kutumiwa na halmashauri ya mji ambao ndiyo wamiliki halali wa majengo hayo. Pia amemwagiza mkurugenzi wa Wilaya ya Bunda kuondoa Ofisi zake maeneo ya mji ili kusogeza huduma karibu na wananchi wake na kutekeleza lengo la uanzishwaji wake. Vilevile kiasi cha shilingi milioni 500 ambazo ni sehemu ya Bilioni 2.14 za mradi wa ujezi wa makao makuu ya halmashauri ya mji ameagiza zirudishwe hazina kwajili ya kusaidia mahitaji mengine?
Katika ziara hiyo mh. Simbachawene amebaini kuwa maeneo ya kiutawala yaliyokuwa yakitengeneza Halmashauri ya Bunda yametenganishwa na eneo la mji hivyo kuleta utata wa eneo la kujenga makao makuu ya halmashauri ya Wilaya. Kutokana ukweli huu ameahidi kuangalia upya uwezekano wa kuongeza maeneo yanayotengeneza Jimbo la Bunda vijijini kuwa sehemu ya halmashauri ya mji wa Bunda.
pia mhemiwa Simbachawene ametumia nafasi hii kuziagiza halmashauri zote nchini kutobadili matumizi ya fedha zozote za miradi bila kipata Kibali cha Ofisi ya waziri wa nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI?
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda