KIKAO CHA DHARURA CHA KAMATI YA AFYA YA MSINGI CHA WILAYA YA BUNDA (PHC)
Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya ya Bunda chini ya Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya Bi. Lydia S. Bupilipili imelazimika kukaa kikao cha dharura kujadili namna ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona unaosabishwa na virusi vya COVID-19.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda amesema serikali imechukua hatua za msingi kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na kutoa matamko mbalimbali ya kutekelezwa nchi nzima ili taifa letu libaki kuwa salama.
Ugonjwa wa Corona tayari umeshaingia nchini na hadi sasa kuna case 12 za wagonjwa wa Corona ambao wapo katika uangalizi wa madaktari.
Lengo kuu la kikao hiki ni kujadili hatua mbalimbali za lazima katika kupambana na ugonjwa huu. Wajumbe walijadiliana kwa kina na kuja na maazimio yafuatayo:-
i. Kuhakikisha elimu dhidi ya ugonjwa wa corona inatolewa kwa jamii na taasisi zote za serikali na zisizo za serikali.
ii. Kuhakikisha vituo vyote vilivyotengwa kwa tahadhari (Karantini) ambavyo ni Bukama, Bitarugu na Mwitende vinajengewa uwezo wa kukabiliana na washukiwa wote wa ugonjwa wa Corona.
iii. Kuhakikisha vituo vyote vya kutolea huduma ya afya vinanunua vipimia joto (Thermoscanner) kwaajili ya kutambua dalili za awali za ugonjwa wa Corona.
iv. Kuwa na maeneo ya kunawia mikono sehemu zote za taasisi, stendi, makanisa, misikiti na maeneo ya biashara.
v. Kufatilia na kuhakikisha bei ya vitakasa mikono inabaki katika bei yake ya msingi kuepuka upandishaji holela wa bei.
vi. Kuhakikisha magari ya abiria yanakua sit level (abiria kulingana na idadi ya viti). Mabasi yasizidishe abiria.
vii. Kuanzisha vyumba tengwa (Holding rooms) kwenye vituo vyote vya afya kwa washukiwa wa ugonjwa wa corona.
viii. Kusitisha uuzaji wa vilevi vyote kwenye maeneo ya mitera, minada na masoko ili kuepusha mazingira hatarishi ya ugonjwa huu.
ix. WDC zote kuandaa program ya kuelimisha umma ikiwezekana kutumia walimu waliopo katika kata zetu kutoa elimu.
x. Kuhakikisha Dawa na vifaa tiba vya ugonjwa wa Corona vinanunuliwa na kuwepo katika vituo vya kutolea huduma.
Mheshimiwa Mkuu wa wilaya Bi. Lydia S. Bupilipili ambae ndie Mwenyekiti wa kikao hiki amesema kupitia viongozi wote wa serikali, kamati ya ulinzi na usalama, Wakurugenzi na watumishi wote pamoja na viongozi wa dini lazima tusimamie na kuhakikisha maazimio haya yanazingatiwa na kutekelezwa na wananchi wote. Usafi uzingatiwe kwani ugonjwa huu unatukumbusha pia suala la usafi.
Aidha tuzingatie maelekezo yote yaliyotolewa na Serikali na wataalamu wa Afya kama vile:-
Kunawa mikono kwa sabuni mara kwa mara.
Kuepuka kushikana mikono.
Kutumia vitakasa mikono.
Kuepuka safari zisizo za lazima.
Kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.
Na Kwenda kituo cha afya mara uonapo dalili za ugonjwa huu.
Tuachane na mira na desturi zinazoshabikia uchafu.
Ugonjwa wa Corona ulianzia nchini China maeneo ya Wuhani mwishoni mwa mwaka 2019. hadi sasa kesi za corona zilizolipotiwa duniani kote ni kesi 471,417. Ugonjwa huu umesababisha vifo vya watu 21,295 na wagonjwa waliodhibitika kupona ni wagonjwa 114,642.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda