Wakazi wa kata ya Wariku wamejawa na furaha baada ya kutembelewa na Mkuu Wilaya Dokta Vicent Anney kuongea nae na kutatua kero zao.
Dokta Naano amewaeleza wananchi wa kata ya Wariku mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Dokta Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dokta Naano amesema kata ya Wariku imepokea zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kwa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya Wariku pamoja na nyumba ya watumishi, ujenzi wa madarasa mapya kabisa na umaliziaji wa maboma mbalimbali ya madarasa.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amewaasa wananchi kuimarisha ulinzi shirikishi kupunguza matukio ya wizi wa maliza na Umma na mali za wananchi. Amewataka wananchi kuchangia vyakula mashuleni kwaajili ya watoto wao na wasiochangia kuchukuliwa hatua kali za kiaheria.
Kuhusu kero ya maji Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema atatuma timu ya watalamu kufanya tathimini itakayoleta utatuzi wa muda mfupi na wa muda mrefu.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ameagiza Idara ya afya kuanza kutoa huduma ya Afya ifikapo tarehe 20 ya Mwezi wa saba mwaka 2023 katika kituo cha Afya Wariku. Na pia ameagiza wazee kupewa vitambulisho vya kupata matibabu bure.
Kwa upande mwingine ameihasa jamii kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake. Na pia amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao.
Amewaelekeza wachimbaji wa madini kuandika barua ya kuomba kupelekewa umeme katika maeneo ya machimbo ili aweze kuwaelekeza TANESCO kupeleka umeme.
Haya ni baadhi ya mambo yaliyojiri leo katika Mkutano wa hadhara wa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda