Jumatano 23.08.2023
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda chini ya Mwenyekiti Mayaya Abraham Magese imefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya Halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na miradi ya Taasisi za Serikali zilizomo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa nia ya kuona utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha miezi sita (Januari-Juni, 2023)
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya Msingi katika Kata ya Nyasura, ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu matatu na bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Mazoezi, Mradi wa jengo la mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri na Bweni la wanafunzi sekondari ya Kunzugu.
Aidha, Kamati imetembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, maeneo ambayo yatajengwa stendi Mpya ya Kisasa na soko jipya pamoja Zahanati ya Rubana.
Kamati imetembelea pia mradi wa umeme katika mtaa wa Mbugani Manyamanyama, Mradi wa Maji wa Misisi Zanzibar, Mradi wa ujenzi wa Mzani wa kisasa wa Rubana, Mradi wa ujenzi wa Ofisi mpya ya TRA pamoja na mradi wa Ujenzi wa barabara inayoelekea Halmashauri ya Mji wa Bunda na mtaa wa Nyasana katika Kata ya Kabasa.
Kamati imeridhishwa na miradi yote na kuielekeza Serikali kukamilisha miradi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Kwa upande miradi iliyobainika kuwa na mapungufu madogo, Kamati imeelekeza kufanyiwa marekebisho.
Mwisho Kamati imeipongeza Serikali chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta miradi ya kutosha katika Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa lengo la kuboresha huduma kwa Wananchi na kuiomba izidi kuleta miradi mingine zaidi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda