Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kukagua maendeleo ya ujenzi ambapo ametoa maelekezo mbalimbali na kuahidi kutembelea tena kuona kama yamefanyiwa kazi.
Mbali na Hospitali, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametembelea shule za Sekondari ambazo zinatarajia kujenga madarasa kwaajili ya Mapokezi ya wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwaka 2025 na tayari zimeshapokea fedha za ujenzi huo. Baadhi ya shule alizotembelea ni shule ya Sekondari Paul Jones, Shule ya Sekondari Migungani na Shule ya Sekondari Dr. Nchimbi.
Katika shule hizo, Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amekagua maeneo ambayo madarasa yatajengwa lakini pia amekagua Miundombinu ya shule yakiwemo madarasa na madawati. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo mbalimbali kwa wasimamizi wa shule hizo ikiwemo kurekebisha madawati yote yaliyoharibika ili yaweze kutumika tena.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda