Halmashauri ya Mji wa Bunda Leo imefanya zoezi la kugawa fedha kwa Walengwa wa Kaya Masikini (TASAF) ikiwa ni Dirisha la mwezi Novemba na Disemba.
Aidha Walengwa wamehamasishwa kutumia njia ya kidigitali kama Benki na Mitandao ya simu katika kupokea fedha kutoka TASAF ambazo ni salama zaidi kwao. Ilikuonesha msisitizo katika hilo Leo pia kulikua na zoezi la kufungua Akaunti Benki kwa walengwa wanaopenda lakini pia kusajili namba za simu kwa wanaopenda njia ya simu.
WALENGWA KAYA MASIKINI WAPEWA ELIMU KUHUSU MASWALA YA KIJINSIA KATIKA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KAYA MASIKINI
Serikali katika Mpango wake wa kuendelea Kunusuru Kaya Masikini, leo kabla kufanya malipo kwa walengwa imetoa Elimu kuhusu masuala mbalimbali ya Kijinsia ambapo imegusia ushiriki wa wanaume na wanawake katika majukumu na mgawanyo wa majukumu sawa katika kuimarisha Pato la familia.
Kwa upande mwingine, walengwa wamefundishwa kuhusu Ukatili wa kijinsia, sababu zinazopelekea ukatili wa kijinsia pamoja na namna ya kushughulikia Ukatili wa kijinsia katika Jamii.
Pichani ni Picha mbalimbali za walengwa wa Kaya Masikini katika Kata ya Nyamakokoto wakipata Elimu kutoka kwa Bi. Editha.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda