Leo tarehe 18.08.2022 Benki ya Biashara Tanzania imeendeleza utaratibu wa kurudisha faida kwa jamii kutokana na faida inayozalisha kwa kuichangia Halmashauri ya Mji wa Bunda Vifaa vya Kielekroniki ambavyo ni Kompyuta Moja na Scanner Moja kwaajili ya kuongeza ufanisi wa kazi.
Akitoa neno la shukrani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bw. Emmanuel J. Mkongo baada ya kupokea vifaa hivyo ameishukuru na kuipongeza Benki ya Biashara Tanzania kwa ushirikiano mzuri inauonesha katika Ofisi yake zaidi kwa kuchangia Hivyo vifaa vya Kielekroniki ambavyo kwa namna Moja au nyingine vitaenda kusaidia kuboresha kutoa huduma kwa Wananchi na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Zaidi ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika Benki hiyo hasa kwa kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa Watumishi na Wananchi wote wa Halmashauri ya Mji wa Bunda. Aidha, Mkurugenzi ameziomba Taasisi nyingine za kifedha kujitokeza na kuiga mfano mzuri wa Benki ya TCB kwa hiki walichokifanya.
Awali Meneja wa Benki ya Biashara Tanzania Tawi la Bunda Bw. Samuel Charles amesema Benki ya TCB imeamua kusaidia Halmashauri ya Mji wa Bunda Vifaa hivi vya Kielekroniki Ili kusaidia kupunguza upungufu uliopo Halmashauri wa vifaa na zaidi kuboresha utoaji wa Huduma Bora kwa Wananchi na kwa Wakati.
Bwana Samuel ameongeza kusema kuwa Benki ya TCB inanufaika na Halmashauri kwa kutoa mikopo kwa Watumishi ambapo Ofisi ya Mkurugenzi ndio inakua mdhamini Mkuu wa Watumishi hao. Mbali na kutoa mikopo kwa Watumishi Benki imekua ikitoa mikopo pia kwa Wananchi wote wenye vigezo.
Mwisho Meneja amesema kuwa mara nyinyi wanarudisha faida kwa Taasisi kwasababu Taasisi inatoa huduma kwa watu wengi zaidi hivyo nao wanakua wanahusika kwa namna Moja ama nyingine kutoa huduma kwa Wananchi.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda