LEO tarehe 02/02/2022, Baraza la Halmashauri ya Mji wa Bunda limepitisha jumla ya shilingi Bilioni 25 kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha ujao 2022/23. Bajeti hiyo imejadiliwa na kupitishwa na Waheshimiwa Madiwani katika Mkutano Maalum wa Baraza la Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Michael Kweka, ameliongoza Baraza hilo kwa kuwapitisha Waheshimwa Madiwani kujadili Mapendekezo ya Makisio ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Waheshimiwa Madiwani wameipitia Mpango na Bajeti hiyo kipengele kwa kipengele na kisha kuipitisha kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kwa mwaka wa fedha ujao 2022/23.
Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. Emmanuel Mkongo amelieleza Baraza kuwa Halmashauri ina mipango madhubuti ya Halmashauri kuongeza Mapato. Pia ameliomba Baraza kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Mapato na Timu za ukusanyaji wa Mapato ili ziweze kutekeleza majukumu yake ya kukusanya mapato kwa ufanisi.
Mkurugenzi ameongeza kuwa endapo mapato ya Halmashauri yataongezeka, Halmashauri itakuwa na wigo mpana na uwezo wa kutekeleza shughuli za maendeleo katika Kata na Mitaa. Hivyo ameomba ushirikiano kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani kudhibiti upotevu wa mapato katika maeneo yao.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda