Kama ilivyo kawaida ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney kukutana na makundi mbalimbali ndani ya wilaya kusikiliza na kutatua kero zao, leo ilikua zamu ya wafanyabiashara.
Mkuu wa Wilaya aliambatana na KUU ya Wilaya,Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tawi la Bunda, Meneja wa TARURA wilaya,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na BUWSSA kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero.
Wafanyabiashara wamempongeza Mkuu wa Wilaya kwa wazo zuri la kuwakutanisha na kusikia kero zao aidha wameeleza baadhi ya kero walizonazo ni kuwekewa mfumo rahisi wa hesabu zao kwa kuzingatia uelewa wa wafanyabiashara, kuboreshewa huduma ya Maji, huduma ya usafi, Barabara, Mfumo wa Tausi wa utoaji leseni, kupewa, taarifa mapema pindi mabadiliko yanapofanyika katika maeneo yao ya Biashara, kuboresha vibanda vya stendi pamoja na stendi mpya, tatizo la kelele kupitiliza, kushirikishwa katika miradi inayotekelezwa na Serikali kwa kupewa zabuni, kulipwa madeni yao na mambo mengine mengi.
Mkuu wa Wilaya alitoa nafasi kwa watalamu kujibu hoja za wafanyabiashara ambapo watalamu walikiri kuzipokea kero hizo na kuzifanyia kazi. Aidha Wakurugenzi wameomba Mahusiano mazuri toka kwa wafanyabiashara, Uaminifu pindi wanapokua wapewa zabuni, kutoa huduma bora yenye viwango vinavyohitajika na kutoa huduma kwa wakati.
Halmashauri zimeahidi pia kulipa madeni kidogo kidogo kulingana na mapato yanayokusanywa. Naye Meneja wa TRA ameahidi kutoa Elimu ya mlipa kodi na mambo mengine yote yanayohusu ulipaji wa kodi ili kuondoa sintofahamu ya inayojitokeza kwa wafanyabiashara. Kuhusu barabara Meneja ameahidi kuzifanyia Kazi.
Mwisho Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Dkt. Vicent Anney amewaahidi wafanyabiasha kwamba matatizo yote yatatatuliwa na Mazingira ya Biashara yatakua bora.
Aidha, Dokta Anney ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya Mji wa Bunda kutenga eneo la Bustani mji itakayowafanya watu kupumzika, kuweka Vyombo vya taka (dust bin) za aina ya chupa, plastic, na taka zinazooza na kuweka mtu wa kuelekeza watu namna ya kutumia.
Mwisho amewataka kufuata sheria ili kuepuka mkono wa Serikali
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda