Dr. Vincent Mashinji Mkuu wa Wilaya ya Serengeti ambae pia anakaimu Ukuu wa Wilaya ya Bunda Leo tarehe 14.11.2022 amewakumbusha Viongozi na wazazi umuhimu wa lishe kwa watoto.
"Ubongo ulio nao sasa asilimia 95 uliupata ukiwa na umri wa miaka mitano" DC Dr. Vincent Mashinji. Ameyasema hayo Wakati akieleza umuhimu wa lishe Bora katika makuzi ya watoto Wakati wa ufunguzi wa Kikao Cha kupanga bajeti ya lishe kwa Mwaka 2023/2024.
Dr. Mashinji amesema tatizo la lishe hivi sasa ni Kubwa na ndio maana unakuta wazazi wanahangaika sana na watoto wao katika kuwaelekeza mambo mbalimbali.
Mashinji amesema takwimu zinaonesha zaidi ya watoto laki Moja na nusu Wilayani Bunda wamedumaa, Hivyo tatizo ni Kubwa na tunatakiwa kukabiliana nalo.
Aidha Dr. Mashinji amesisita sana matumizi ya vyakula vyenye madini ya folic acid na Iodine kwa watoto Ili kuwafanya kuwa na Afya ya akili iliyobora.
Baada ya kufungua Kikao hicho Wataalamu wa lishe toka Wizarani na Mkoani pamoja na Watumishi wa Halmashauri zote mbili Bunda Mji na Bunda Wilaya waliendelea na Kikao Cha majadiliano ya namna gani ya kupanga bajeti ya lishe iliyobora katika Wilaya ya Bunda.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda