Halmashauri ya Mji wa Bunda imepokea msaada wa mifuko 300 ya saruji vyenye thamani ya Sh 6,000,000/= toka kwa kampuni ya kizalendo ya MWANZA HUDUMA; kwajili ya kuchangia ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi za Kabarimu na Bitaraguru. Katika kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa kampuni ya MWANZA HUDUMA ameeleza kuwa kampuni yake ina utaratibu wa kuthamini na kurudisha fadhila kwa jamii. Pia kaahidi kuendelea kuchangia maendeleo katika wilaya ya Bunda mara anapopata nafasi ya kufanya hivyo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi saruji Makamu Mwenyekiti wa halmashauri aliishukuru kampuni ya Mwanza Huduma na kuwapongeza sana kwa kuwajali watoto wa Bunda
kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ili kutoa elimu bora. Aidha amewataka wadau wengine wa maendeleo walioko ndani na nje ya mji wa Bunda kuiga mfano huo wa kujitolea kuchangia maswala mbalimbali ya maendeleo katika halmashuri.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda