Halmashauri ya Mji wa Bunda imepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya Sh 15,722,000/= toka kwa kampuni ya kizalendo ya Maboto Enterprise Limited; kwajili ya kuchangia ujenzi wa jengo la kuhifadhia maiti. Katika kukabidhi msaada huo Mkurugenzi wa kampuni ya Maboto Bw. Robert Maboto ameeleza kuwa kampuni yake ina utaratibu wa kuthamini na kurudisha fadhila kwa jamii. Pia kaahidi kuendelea kuchangia ujenzi wa jingo hilo mpaka litapo kamilika. Vifaa alivyo kabidhi katika hafla hiyo ni kama ifuatavyo:- Mbao 725 za ukubwa tofauti, Bati 28G 216, Nondo 90 za ukubwa tofauti, saruji mifuko 50, misumari kilo 182 ya ukubwa tofauti, binding wire 1, kenchi wire1 pamoja na usafiri hadi eneo la ujenzi.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo Mkuu wa wilaya ya Bunda Bi. Lidia Bupilipili amesema kukamilika kwa jingo hilo la kuhifadhia maiti italeta tija kubwa kwa wananchi wa halmashauri ya mji wa Bunda, wilaya ya Bunda na majirani zao, ameeleza kuwa wananchi wa Bunda wamepata adha kwa kipindi kirefu maana wamekuwa wakifuata huduma hiyo mbali sana na kwa gharama kubwa pale wapendwa wao wanapoaga dunia. Hivyo ameipongeza kampuni ya Maboto kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wake.
Awali akimkaribisha Mkuu wa wilaya Mkurugenzi wa Mji wa Bunda Bi. Janeth Mayanja ameipongeza kampuni ya Maboto kwa kuunga mkono juhudi za serikali za kuimarisha miundombinu ili kutoa huduma za afya zilizo bora. Aidha amewataka wadau wengine wa maendeleo walioko ndani na nje ya mji wa Bunda kuiga mfano huo wa kujitolea kuchangia maswala mbalimbali ya maendeleo katika halmashuri.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda