MTAKUWWA ni Mpango kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto. Mpango huu hutekelezwa katika ngazi mbalimbali ndani ya Jamii. Leo Kamati za MTAKUWWA ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, zapewa mafunzo kwa ufadhili wa Kanisa la K.K.T kupitia mradi wa Kizazi Hodari na shirika la Rafiki SDO.
Mafunzo haya yameanza Leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda na yatadumu kwa muda wa siku Tatu. Lengo la Mafunzo haya kuzijengea Kamati uwezo wa kupambana, kutokomeza na kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto.
Akifungua Mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bwn. Ladislaus Magaso amesema Kamati hizi zinatakiwa kuwepo katika Kata zote za Halmashauri ya Mji wa Bunda lakini kwa kuanza mafunzo yataaza katika Kata Tano na baadae kufikia Kata zote.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda