Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo amefanya Kikao na Watendaji wa Kata 7 za Katikati ya Mji lengo likiwa kuwakumbusha baadhi ya sheria ndogo za Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Baadhi ya mambo waliyokumbushwa ni kusaidia kusimamia na kuzuia upotevu wa mapato katika vyanzo mbalimbali vilivyopo maeneo yao kama vile ushuru wa madini ujenzi, vibali vya ujenzi pamoja na vyanzo vinginevyo vinavyopatikana katika maeneo yao.
Mkurugenzi amewakumbusha pia kusimamia suala la usafi wa mazingira kwa kudhibiti utupati wa taka hovyo, kuzuia na kukamata mifugo inayozurura, kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao pamoja na kudhibiti kelele zinazozidi kipimo.
Aidha Mkongo amewataka Watendaji kuzingatia nidhamu na maadili ya kazi, kuhamasisha wananchi kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao, kuelimisha na kutoa tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza.
Mwisho amewataka Watendaji kuwa wabunifu katika kutafuta wadau mbalimbali wa kuchangia maendeleo na pia kushirikisha ofisi yake na kuomba ushauri juu ya wadau wanaojitokeza kusaidia kitu fulani au uwekezaji katika maeneo yao ili kuweka mazingira ya usalama pande zote.
Kata Saba zilizoshiriki kikao hiki ni kata ya Bunda Mjini, Nyasura, Manyamanyama, Kabarimu, Balili, Nyamakokoto na Bunda stoo.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda